Serikali imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi na
sheria ya uchaguzi bila kujali mchakato wa mabadiliko ya katiba
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amesema pia kunatakiwa
tume huru ya uchaguzi ambayo itafanya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 uwe huru na
haki.
Kiongozi huyo amesema kuwa huenda mabadiliko ya katiba
yasifanyike kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu
2015 hivyo mabadiliko ya sheria zilizopitwa na wakati ni muhimu bila
kujali kukamilika kwa mchakato wa
katiba.
Bwana Mbowe amesema mabadiliko ya uchaguzi yasipofanyika
kutatoa taswira tofauti hivyo angalizo ni kufanya mabadiliko kwani wananchi
wamechoka kuyumbishwa na tume ya uchaguzi ambayo amedai siyo huru.
0 comments:
Post a Comment