Kikosi cha Simba
Uongozi wa klabu ya Simba umetoa wiki moja kwa beki wake Juma Nyosso kujiunga na kikosi cha SIMBA B ili kutekeleza masharti ya adhabu ya utovu wa nidhamu ambao aliuonesha.

Afisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema kuwa kitendo cha beki huyo kutofanya mazoezi na Simba kwa madai kuwa mkataba wake hauruhusu kufanya hivyo ni kitendo kinachoashiria kutokomaa kisoka.

Kuhusu madai ya Nyosso kutaka kuvunja Mkataba,'Leo ukiruhusu Nyosso kuvunja mkataba na Simba,kesho atakuja kapombe atataka kuvunja mkataba keshokutwa Juma Kaseja ni vitu havikubaliki kama Nyosso anataka kuvunja mkataba kuna hatua za kisheria anatakiwa kufuata,vinginevyo tukiruhusu vitu kama hivi tutajikuta hatuna timu aliongeza Afisa huyo'.

Katika hatua nyingine Kamwaga amesema kuwa Suala la utovu wa nidhamu wa kiungo Haruna Moshi Boban wamemwachia Jukumu Ismail Aden Rage ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Simba na kutoa fursa ya kurejesha mawasiliano mazuri kati ya uongozi na kiungo huyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top