
Mlima Ontake
Takriban wakwea milima 30 huenda
wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku
ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na
kilele cha mlima huo.
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha mlima Ontake.

Waokoaji hao wamefanikiwa
kufika kwenye kilele cha mlima huo ambapo ndege ya kijeshi aina ya
helikopta ilitumiwa kuwaokoa karibu watu 40 waliokuwa wamejeruhiwa.
Zaidi
ya wakwea milima 200 walifanikiwa kuteremka kutoka kwa mlima huo wenye
urefu wa mita 3000 wakati mlima huo ulipoanza kutupa mawe na majivu bila
ya kutoa tahadhari yoyote.
Baadhi yao walisema kuwa walishindwa kupumua kutokana na majivu yaliyokuwa yakianguka kutoka angani.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment