Wachunguzi wa Kijerumani dhidi ya ndege ya abiria ya Malaysia ambayo ilipata ajali huko Ukraine mwezi July na kuripuka angani wanaeleza kuwa ndege hiyo baada ya kukumbwa na kitu chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali ndio chanzo cha ajali.

Mwandishi wa BBC amesema kwamba ushahidi huo ni wa wazi na kwamba ndege hiyo ilishambuliwa kwa kombora.

Katika ripoti yao ya kwanza ya kiuchunguzi, maafisi wa Kijerumani katika masuala ya usalama wa anga wameeleza kuwa hakukuwa na tatizo la kiufundi lililosababisha ndege hiyo ipate ajali, ama makosa ya rubani yalosababisha ndege aina ya MH17 kuripuka.

Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurikodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikuwa na dharura.

Abiria wote miambili na tisini na nane walipoteza maisha. Ndege hiyo ilitoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur. kutokana na ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua ndege hiyo. Hata hivyo, mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na ajali hiyo.
Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 inaweza kupatikana pindi mwakani.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top