Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun
Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa
kiislamu Boko Haram.
Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa
siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana
kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa
ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.
Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri.
Wakazi
wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao,
wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo
kufungwa.
Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment