Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
YAHAYA unaishi wapi? Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.
YAHAYA unaishi wapi? Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.
Tukio hilo lilitokea Septemba 19 mwaka huu katika Kituo cha Afya cha
Kimara baada ya tapeli huyo kumlaghai dada mmoja aitwaye Wema Raymond
wakutane hapo kwa ajili ya vipimo vya ukimwi vilivyotakiwa
kuambatanishwa katika fomu ya kuomba nafasi ya kazi ambayo awali dada
huyo alidai kupatiwa na tapeli huyo.
Akizungumza na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo
kupitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye
awali alipigiwa simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi.
Wema alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku
chache baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi
katika Chuo cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo.
“Kwa sababu Rebecca ana kazi yake tayari
aliamua kunitaarifu mimi kwa kuwa anajua natafuta kazi,” alisema
Wema.Alisema alikutana na jamaa huyo ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa
fomu aliyoelekezwa kujaza kisha akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama
malipo ya fomu hiyo na gharama za mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu
kazi, fedha ambazo hakuwa nazo kwa muda huo na kulazimika kumuomba
rafiki yake Rebecca amsaidie.
“Baada ya kumaliza mazungumzo pale chuoni akanisindikiza hadi nje,
lakini cha kushangaza pale mlangoni nikamuona anampatia mmoja wa walinzi
hela, nikamuuliza kwa nini aliwapa hela, akasema eti watu wengi
wanaitaka nafasi ile wakiwemo walinzi hao, hivyo alikuwa akiwapoza
wasimsemee kwa kunitafutia mimi kazi isije akafukuzwa kazi,” alisimulia
Wema na kuongeza kuwa alitakiwa kesho yake kupima VVU ili vipimo hivyo
viambatanishwe kwenye barua yake ya maombi.
Katika Kituo cha Afya Kimara, alikutana tena na tapeli wake,
aliyeonekana kuwasalimia madaktari na manesi kana kwamba wanajuana kisha
akaingia kwa dokta na kuzungumza naye.Baada ya muda tapeli huyo alitoka
nje kisha akamwambie Wema aingie kwa daktari kwa ajili ya kujaziwa
fomu hizo kienyeji bila kupimwa maambukizi ya ukimwi.
“Nikiwa ndani machale yalinicheza, ikabidi nimuulize yule daktari
kama anajuana na yule jamaa, daktari akasema kwamba hawafahamiani hata
kidogo jambo lililonishtua. “Nikamnong’oneza kuwa nahisi kutapeliwa,
akaniambia nikakae naye nikijifanya namuongelesha huku yeye akizunguka
kwa mlango wa nyuma na kuwaita mapolisi.
“Katika upekuzi alikutwa na zile pesa zangu za jana zikiwa kwenye
simu yake na shilingi 90,000 akiwa nazo mfukoni huku akionekana kutumia
simu yenye jina la Martha Peter ambalo mwenyewe alikiri kuwa alikuwa
akinitapeli.”
“Polisi walichukua maelezo yangu na kufungua jalada RB/4969/2014
KUJIPATIA PESA KIUDANGANYIFU kisha wakaniambia nifike kesho yake,”
alisema Wema na kuongeza kuwa siku ya pili alipofika kituoni hapo
aliwakuta watu wengine waliodai kutapeliwa na jamaa huyo kwa majina
tofauti na walipopiga hesabu fedha alizowatapeli kwa pamoja zilifikia
sh.1,435,000.
GPL
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment