Mahakama nchini Jordan haijampata na
hatia ya tuhuma za kigaidi Mhubiri wa kiisilamu anayesemekana kuhubiri
itikadi kali Abu Qatada.
Jopo la majaji wa kiraia waliokuwa katika
mahakama hiyo, hawakumpata na hatia yoyote bwana Qatada kutokana na
madai kuwa alihusika na njama iliyotibuliwa ya kushambulia sherehe za
mwishoni mwa mwaka 2000.
Uamuzi huo umetolewa baada ya Abu Qatada
kutopatikana na hatia mwezi Juni katika kosa lengine la kupanga njama ya
mashambulizi mwaka 1998 nchini Jordan.
Abu Qatada alitimuliwa kutoka Uingereza mwezi Julai mwaka 2013 kwa madai ya kueneza itikadi kali.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment