Benjamin Mkapa
NINAFURAHI na kushukuru kwa kupata fursa hii ya kutoa salamu na
pongezi zangu za dhati kwa Rais mstaafu Daniel Toroitich arap Moi wakati
akitimiza umri wa miaka 90. Hakika Moi ni nembo, mtu mashuhuri na
kizazi adimu cha viongozi wa Afrika.
Kwa karibu miaka minane, tulifanya kazi kwa karibu na kwa amani kama
viongozi wa nchi zetu; Kenya na Tanzania, na katika muktadha wa Ukanda
wa Maziwa Makuu, kukuza maendeleo na kuimarisha amani na utulivu.
Tangu mwanzo kabisa, Rais Moi alionekana akiibukia kuwa mmoja wa
viongozi wakubwa wa Afrika Mashariki na rais aliyeitumikia Kenya kwa
muda mrefu zaidi.
Hicho ni kielelezo cha kweli cha mtu kubahatisha kuzaliwa ili kuongoza, na hivyo kujikuta mzigo wa uongozi ukiwa mabegani mwake.
Rais mwasisi wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta, alimbaini mwalimu huyu wa
shule akiwa mnyenyekevu na asiyejikuza na kumfanya kuwa makamu wake wa
rais kwa miaka mingi.
Moi alionyesha umahiri wake wa uongozi wakati wa harakati za
kupigania uhuru wa Kenya na alianzisha uhusiano na viongozi wa vuguvugu
za kudai uhuru Afrika Mashariki.
Wakenya wako kwenye nafasi nzuri ya kushukuru mchango wake kwa maendeleo ya taifa.
Walio nje ya taifa hilo, hata hivyo wanaona jinsi alivyofanya kazi ya
kupanua mfumo wa elimu kwa ajili ya fursa sawa kwa watoto wote.
Na kwa siasa za mstari wa mbele, watakuwa wanakumbuka namna
alivyokuwa na maono wakati alipoanzisha na kusimamia mfumo wa vyama
vingi vya siasa na serikali.
Kwa kufanya hivyo, aliweza kuifanya Kenya ijitegemee kwa miaka 10 bila msaada wa kigeni au wa maendeleo.
Kwa upande wangu, nampigia saluti Rais Moi kwa mambo makubwa mawili
ya kukumbukwa; mchango wake kwa amani na utulivu wa eneo la Maziwa Makuu
na kufufuliwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais Moi kwa muda mrefu amekuwa mtengeneza na mjenga amani asiyechoka.
Kumbukumbu zinaonyesha namna alivyojishughulisha kikamilifu katika
utafutaji wa suluhu ya migogoro katika Pembe ya Afrika, nchini Ethiopia,
Uganda, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan ya zamani na
Sudan Kusini ya sasa.
Rais Moi atakumbukwa kwa juhudi zake zilizosababisha ufufuaji wa EAC, ambayo ilivunjika mwaka 1977.
EAC ya leo ni matunda ya ushawishi wake na inatoa fursa zisizo na
kikomo kwa watu wa Afrika Mashariki kujenga msingi imara wa ushirikiano
wa kiuchumi na utangamano.
Kaka yangu mkubwa na kiongozi mwenzangu wa zamani, anaweza kuangalia
nyuma akiwa ameridhika kwa utumishi uliotukuka wa aina yake na usio na
kifani kwa Kenya na Afrika.
‘Happy Birthday’ Rais Moi.
Mtanzania
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment