Rais Barrack Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama ametangaza mpango
wake wa kuwatuma wanajeshi 3,000 Afrika Magharibi njia moja ya kusaidia
katika vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Rais Obama ametoa
wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kuzuia kuenea kwa
ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika ambao unaenea kwa kasi sana.
Bwana
Obama amesema kuwa iwapo mlipuko wa maradhi hayo haukomeshwi kwa sasa,
mamia ya maelfu ya watu wataambukizwa na yatakuwa tishio kwa usalama wa
dunia.
Jemedari mmoja wa Marekani amewasili nchini Liberia
kuongoza wanajeshi hao 3,000 wa jeshi la Marekani waliotumwa eneo hilo
kupambana na maradhi hayo.
Wanajeshi hao watasimamia ujenzi wa
vituo vipya vya kimatibabu na pia watahusika katika utoaji wa mafunzo ya
kimatibabu kwa wahudumu.
Kumekuwa na malalamishi kwamba jamii ya
kimataifa imelegea katika harakati za kukabiliana na mlipuko wa Ebola
katika mataifa ya Afrika magharibi.
Mataifa ya Sierra Leone,
Liberia na Guinea ndiyo yaliyoathirika zaidi huku zaidi ya watu 2,400
wakiwa tayari wamepoteza maisha yao kufikia sasa.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu ni raia wa Liberia.
Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha kuwa huenda watu zaidi wakazidi kufariki.
Umoja
wa Mataifa (UN) unapangiwa kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa Ebola katika mkutano unaopangiwa kufanyika huko Geneva.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment