Polisi Uganda wamewakamata washukiwa 19 wa Alshabab
Polisi nchini Uganda wanasema kuwa wamekamata kiasi kikubwa cha vilipuzi walipokuwa wakifanya operesheni ya kutibua jaribio la shambulizi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabab.

Hadi sasa, watu kumi na tisa wamekamatwa na polisi na wanahojiwa kuhusiana na nia yao kutekeleza vitendo vya kigaidi, kulingana na msemaji wa polisi.

Wiki iliyopita, ubalozi ya Marekani mjini kampala ulionya kuwa kulikuwa na uwezekano wa shambulizi la kulipiza kisasi mauaji wa kiongozi wa kundi hilo la Alshabab.

Uganda inalaumiwa kwa kutoa majeshi yake kupigana chini ya nembio ya Umoja wa Afrika Amisom.

Polisi Uganda wamewakamata washukiwa 19 wa Alshabab
Marekani ilitangaza kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Alshabab Ahmed Abdi Godane baada ya shambulizi la angani Septemba 2 .
Serikali inasema kuwa kundi hilo la kigaidi lilikuwa limepanga mashambulizi mji mkuu wa Kampala.

Askari walisema kuwa kundi hilo lilikuwa limepangia mashambulizi katika miji mingine mwishoni mwa wiki.

Siku ya Jumapili, Marekani iliondoa onyo lao ikidai kuwa iliamini kuwa tishio la shambulizi lilikuwa limeondoka.

Waziri wa habari nchini Uganda, Rose Namayanja aliwasihi wananchi kuendelea kuwa waangalifu huku serikali ikiendelea kufanya uchunguzi wa mashambulizi iliyokuwa imepangwa.

Alisema kuwa watuhumiwa walikuwa wamepatikana na vifaa vya vinavyohusiana na vitendo vya kigaidi na nia yao ilikuwa wazi sana.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top