Mwanamama raia wa Sudan aliyesamehewa adhabu ya kifo
baada ya kubadili dini amesafirishwa hadi nchini Italia baada ya kuwa
kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake
waliondoka na ndege ya serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa
nchini Italia Lapo Pistelli.
Baba wa Meriam ni muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini hiyo nchini Sudan Meriam pia ni muislamu na hawezi kubadili dini.
Meriam mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa muislamu.
Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia,
aliweka picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema
kuwa wanaelekea kutua mjini Roma.
Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo, ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani.
Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi
May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha
ghadhabu dunia nzima.
Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment