Madaktari nchini India wametumia
saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye
umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .
Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo
na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na
linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha
jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka
30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna
hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali
kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi
kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa
tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno
232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya
kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai
amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu
ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na
ndipo wakamleta Mumbai.
BBC
0 comments:
Post a Comment