Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Dar es Salaam, Paulo Mwandemre (30) amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu kifuani na ‘vibaka’.
Tukio hilo lilitokea jana saa 7.00 mchana wakati Mwandemre alipokuwa akitoa darasani kutimiza majukumu yake.
Mkuu wa Shule hiyo, Macelina Kimario alisema
vijana hao walikuwa wakizungumza na wanafunzi ndipo Mwandemre alikwenda
kuwauliza wanafunya nini.
“Alipowauliza wanafanya nini ndipo kulitokea
kutokuelewana na aliwakamata wote wawili na alipokuwa akiwapeleka
ofisini ndipo mmoja aliyekuwa na kisu akakitoa na kumchoma kifuani,”
alisema Kimario.
Aliongeza: “Mara baada ya kumchoma mmoja
alikamatwa na mwingine alikimbia huyu aliyekamatwa tulimweka ndani na
wanafunzi walikuwa wakimtaka ili wamwadhibu lakini tuliwazuia hadi
polisi walipofika na kumchukua. Mwalimu alipelekwa katika Hospitali ya
Zakiem na baadaye alihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa
matibabu.
Mwandishi wa habari hizi alimkuta Mwandemre akiwa amelazwa wodi namba saba na hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri.
“Sitaki kuzungumza na waandishi..... mimi sitaki wala kupigwa picha......niacheni,” alisema Mwandemre akiwa wodini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo
alisema vijana hao wawili walikuwa eneo la shule na walipomuona
Mwandemre akipita na mfuko mdogo walimvamia na kuuchukua.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment