Askofu Mkuu wa Kanisa
Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinal Pengo
Askofu Mkuu wa Kanisa
Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinal Pengo amesema
shughuli za mchakato wa Katiba zifanyike kwa amani na kwamba ziwalinde
Watanzania katika umoja na mshikamano waliyokuwa nao.
Pia, amewataka wajumbe wa Bunge Maalum
la Katiba kuweka masilahi yao kando na kutanguliza masilahi ya taifa
kwa faida ya Watanzania.
Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa
Katisa Katoliki Magomeni, Kardnali Pendo alisema ni vyema viongozi
wakafahamu kwamba Watanzania ni watu wanaopenda amani, na kwamba yeye
angepAenda kuona amani iliyopo inadumu.
Alisema: "Niseme kwamba, shughuli za mchakato wa kuandika Katiba Mpya zifanyike kwa amani."
Aliongeza: "Ni vyema tukatambua kuwa
Watanzania ni wapenda amani, hivyo wasingependa kuona kukijitokeza
tofauti kati ya wajumbe wa Bunge hilo,"
Alisema kama tunataka nia ni kupata
katiba bora, ni lazima wajumbe wabunge la Maalum la Katiba kuweka
masilahi yao kando na kuangalia yale ya taifa kwa faida ya Watanzania
wote.
Alitoa mfano kwa baadhi ya vingozi wa
nje ya nchi wanavyotambua mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere kwa kuwa ni mtu aliyependa amani, umoja na mshikamamno.
Alisema leo (jana) alifuatilia vyombo
vya habari na kusikia kuwa Rais wa Zimbabwe (Robert Mugabe) akimuelezea
Mwalimu Nyerere kama kiongozi shupavu aliyeweka misingi ya amani
Tanzania kwa kuwa alikuwa mpenda amani.
Naye, Paroko wa Kanisa hilo Joseph
Matumaini alisema Kanisa hilo limejengwa kwa ghalama ya Sh1.25 bilioni
fedha ambazo zimetokana na michango ya waumini wao.
Alisema: "Kanisa hili limejengwa kwa
jitihada za waumi kwa kujitolea, na kwamba tunawashukuru wote kwa
kuijenga nyumba ya mungu,"
Alisema Kanisa hilo lina uwezo wa kuchukua waumini 1500.
Chanzo, mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment