Julius Mtatiro
Jana waziri Maghembe amewaita wawakilishi wa wafugaji waliomo kwenye bunge la katiba, amewaandalia chakula cha kutosha, vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine, huku wakipewa bahasha za nauli baada ya vikao hivyo vya siri.
Waziri wa Elimu Shukuru Kawambwa pia, jana amewaita wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu walioko katika bunge la katiba na kuendelea na mchezo huo.

Mhe. Lowassa pia leo anakutana na wafugaji na wakulima walio wajumbe wa bunge la katiba kwa mfumo huohuo.

Hoja zao wanapokutana na makundi haya ni kupigia chapuo kura ya WAZI na kupinga ya siri, huku wakieleza namna CCM inavyopinga baadhi ya mapendekezo muhimu yaliyomo katika rasimu ya katiba.

Walichofanya mawaziri hawa ndicho kinachofanywa na mawaziri wengine wa CCM, ni agizo la lazima ambalo hivi sasa linatumika hapa Dodoma.

CCM ni chama kikubwa na kikongwe. Rais wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ndiye alitangaza na kuanzisha mchakato wa katiba, mabilioni ya fedha yametumika kukusanya maoni ya wananchi na yametumika pia kuilipa tume, kuitisha mabaraza ya katiba na mabilioni yametumika kuitisha bunge maalum ya katiba.

Leo, CCM na mawaziri wao wanatumia fedha na kutoa rushwa ili kupitisha matakwa yao. Masuala haya yana ushahidi, kesho nitayasema bungeni kwa uwazi kabisa.

Tutasimamia KWELI!
FB 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top