TAARIFA MUHIMU KWA WAAFUNZI WALIOCHAGULIWA KWENDA MASOMONI MSUMBIJI (TAMOSE 2014)

1.    Wanafunzi wote waliochaguliwa kwenda Msumbiji 2014 wanataarifiwa kuwa Mafunzo ya Lugha ya Kireno yataanza wiki ya kwanza ya mwezi Februari 2014 kule Msumbiji. Hivyo watasafiri kwa makundi mawili. Kundi la kwanza litakalokwenda Inhambane litaondoka Jumatano tarehe 29/01/2014. Kundi la pili litakalokuwa Maputo litaondoka Jumapili tarehe 2/02/2014.

2.    Orodha ya majina na tarehe za kuondoka zimeoneshwa hapa chini. Kila mwanafunzi ahakikishe anakata tiketi ya ndege kwa tarehe alizopangiwa. (Wawasiliane na Bodi ya Mikopo kuhusu ununuaji wa tiketi).

3.    Mkutano wa kuwaaga wanafunzi utaofanyika katika chumba cha mikutano cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi tarehe 27/01/2014 saa 4:00 asubuhi. Wote waliochaguliwa wanatakiwa kuhudhuria mkutano huo wakiwa tayari kwa safari kwa tarehe zilizotajwa.

4.    Wanafunzi ambao hawakuomba mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu mwaka huu, itabidi wasubiri maelekezo kupitia namba za simu walizoandika wizarani wakati wa kutuma maombi. 

IDARA YA ELIMU YA JUU

10/01/2014
  Bofya hapa kupata majina Bofya hapa kupata majina
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top