Maelfu ya watu wanaandamana katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumtaka Rais wa mpito nchini humo Michel Djotodia, ajiuzulu.
Hatma ya Djotodia kama Rais wa mpito imejadiliwa
na baraza la mpito la nchi hiyo ambalo limekuwa likikutana nchini Chad
kabla ya mkutano wa viongozi wa kikanda kufanyika.
Rais Djotodia amekosolewa vikali kwa
kukosa kusitisha mapigano ya kidini kati ya wakristo na waliokuwa waasi
waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi
mwaka jana.
Baraza lote la mpito katika Jamuhuri ya Afrika
ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa Afrika wanakutana
kujadili mzozo wa taifa hilo unaoendelea .
Mkutano huo wa viongozi wa kikanda, uliahirishwa, mapema asubuhi Ijumaa.
Lakini wajumbe kwenye mkutano huo wanasema
walitakiwa kuendelea na mkutano usiku kucha ili kubuni mkakati kuhusu
mustakabali wa rais wa taifa hilo Michel Djotodia.
Bwana Djotodia anakabiliwa na shinikizo kali kwa
kukosa kusuluhisha mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchi humo kati ya
wakristo na waisilamu, lakini msemaji wake amesema kuwa hawezi kujizulu.
Viongozi wa kikanda wanasema wajumbe mia moja na
thelathini na watano waliitwa kwa mkutano huo kwa sababu ni raia wa
nchi hiyo pekee wanaoweza kuamua hatma ya taifa lao.
Ghasia baina ya wanamgambo wa kiislam na kikristo zimesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Djotodia aliingia mamlakani baada ya mapinduzi
ya kijeshi mwezi Machi mwaka jana hali iliyotumbukiza taifa hilo katika
viya vya wenyewe kwa kwenyewe.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment