Jeshi la Kenya linalopambana na kundi la wanamgambo
la Al-Shabaab linasema angalau wapiganaji 30 wa kundi hilo wameuawa
Kusini Magharibi mwa Somalia.
Msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir
ameelezea kuwa jeshi la Kenya lilishambulia kwa mabomu mojawapo ya kambi
za kundi hilo katika eneo la Gedo , Alhamisi Jioni.
Aliongeza kwamba miongoni mwa waliofariki ni makamanda kadhaa wa kundi hilo.
Al Shabaab hata hivyo hawajatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Kadhalika Al Shabaab walikiri kufanya shambulizi
la kigaidi mjini Nairobi mwaka jana dhidi ya jengo la kifahari la
Westgate na kuwaua watu 70.
Kenya imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi
hilo tangu mwaka 2011 Oktoba wanajeshi wake walipojiunga rasmi na vikosi
vya muungano wa Afrika ambavyo tayari vilikuwa nchini Somalia kwa kazi
hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa majeshi ya
Kenya yataendelea va vita dhidi ya wanamgambo hao tangu waliposhambulia
Kenya mwaka jana.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment