Rais wa mpito wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Michel
Djotodia, amejiuzulu kufuatia shinikizo kali na kukosolewa kwa mwendo
wake wa kujikokota katika kusuluhisha mgogoro wa kidini unaotokota
nchini humo.
Hatma ya Djotodia ilikuwa swala kuu katika ajenda ya mkutano wa viongozi wa kikanda kuhusu mzozo unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo ulifanyika nchini Chad huku maelfu wakiendelea kutoroka nchini humo kutokana na ghasia.
Maelfu ya watu waliandamana leo katika barabara za mji mkuu Bangui kumtaka Rais Djotodia, ajiuzulu.
Rais Djotodia amekosolewa vikali kwa kukosa
kumaliza mapigano ya kidini kati ya wakristo na waliokuwa waasi
waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi
mwaka jana.
Baraza lote la mpito katika Jamuhuri ya Afrika
ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa Afrika wanakutana
kujadili mzozo unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo wa viongozi wa kikanda, uliahirishwa, mapema asubuhi Ijumaa.
Lakini wajumbe kwenye mkutano huo wanasema
walitakiwa kuendelea na mkutano usiku kucha ili kubuni mkakati kuhusu
mustakabali wa Djotodia.
Viongozi wa kikanda wanasema wajumbe mia moja na
thelathini na watano waliitwa kwa mkutano huo kwa sababu ni raia wa
nchi hiyo pekee wanaoweza kuamua hatma ya taifa lao.
Ghasia baina ya wanamgambo wa kiisilamu na kikristo zimesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Djotodia aliingia mamlakani baada ya mapinduzi
ya kijeshi mwezi Machi mwaka jana hali iliyotumbukiza taifa hilo katika
viya vya wenyewe kwa kwenyewe.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment