Waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Jaji, Georgeb Liundi nyumbani kwake
Keko jijini Dar es Salaam jana. Jaji huyo anatarajiwa kuzikwa keshokutwa kwenye
makaburi ya Chang'ombe.
Taifa limepoteza watu wawili mashuhuri. Hao ni Msajili wa Kwanza
wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji George Liundi (78) na Mbunge wa
zamani wa Dodoma Mjini, Hashim Saggaf.
Jaji Liundi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana
alipokuwa akipelekwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu wakati
Saggaf, ambaye alikuwa Diwani wa Mtafukoge, Dar es Salaam alifariki jana
saa nne asubuhi kwenye Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
Saggaf alizikwa jana kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na mazishi ya Jaji Liundi yamepangwa kufanyika keshokutwa.
Jaji Liundi
Jaji Liundi alikuwa Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, mwaka mmoja baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, Julai
mosi, 1993 na alistaafu mwaka 2001 na nafasi yake kuchukuliwa na John
Tendwa ambaye naye alistaafu Agosti, mwaka jana na kumuachia kijiti,
Jaji Francis Mutungi.
Wakati akiianza kazi hiyo, mfumo wa vyama vingi
ulikuwa hauna nguvu, huku vyama vya siasa vikiwa vichache na kikubwa cha
upinzani kilikuwa NCCR-Mageuzi.
Akizungumza jana nyumbani kwa marehemu, Keko Juu,
Dar es Salaam, msemaji wa familia ambaye pia ni mtoto wa kwanza wa
marehemu Liundi, Taji alisema baba yake kwa muda mrefu alikuwa
akisumbuliwa na maumivu ya mgongo.
Alisema alikuwa ni mtu mwenye afya njema, lakini siku tatu zilizopita alikuwa akilalamika zaidi kuumwa mgongo.
“Afya yake ilikuwa nzuri licha ya kuwa alikuwa
akisumbuliwa na shinikizo la damu (BP), alikuwa akipatiwa matibabu kila
alipokuwa akijisikia vibaya, kifupi alikuwa katika hali nzuri,” alisema
Taji na kuongeza:
“Ijumaa na Jumamosi iliyopita nilimpeleka kwa
daktari wake na kupatiwa matibabu. Jumapili (juzi) aliamka akiwa na afya
nzuri,” alisema Taji.
Alisema hali ya Liundi ilibadilika ghafla usiku wa
kuamkia jana, huku akiwa analalamika kuumwa mgongo... “Niliamua
kumpeleka TMJ lakini tukiwa njiani, alifariki dunia.”
Taji alisema sasa wanasubiri ripoti ya madaktari,
lakini wanaamini ugonjwa uliomuua baba yao ni malaria kali. Alisema
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Alisema misa ya kumuombea Jaji Liundi itafanyika kwenye Kanisa
Katoliki Chang’ombe wilayani Temeke, Alhamisi na mazishi yatafanyika
katika Makaburi ya Chang’ombe.
Marehemu Liundi ameacha watoto watatu na mjane mmoja.
Jaji Liundi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 1980.
Pia amefanya kazi katika nchi mbalimbali zikiwamo Zambia, Zimbabwe na Uswisi
Alikuwa mmoja wa Watanzania waliotengeneza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.”
Wanasiasa wamlilia
Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei alieleza kustushwa
na taarifa za msiba huo na kusema anakumbuka ushirikiano wake kwa vyama
vya siasa.
“Nawapa pole ndugu zake, watoto na mkewe kwa
kumpoteza mtu muhimu, hiyo ndiyo njia tutakayopitia wote. Liundi alikuwa
mtu mwadilifu nasikitika sana kusikia kifo chake,” alisema Mtei.
Kwa upande wake, Tendwa alisema Liundi anapaswa
kuenziwa na Watanzania wote kwa kuasisi mfumo wa demokrasia ya vyama
vingi... “Watanzania wanatakiwa kumpa heshima kwa sababu yeye ndiye
aliyeasisi mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na michakato yote,
zikiwamo sheria mbalimbali zilizopo hadi sasa.
“Yeye ndiye aliyesajili vyama vya awali vya
upinzani mbali na CCM vikiwamo CUF, Chadema, TPP ambacho baadaye
kilifutwa na vingine vingi. Alisimamia chaguzi za awali tangu mwaka 1994
hadi 1995. Alijitahidi kuubeba mfumo huo ukiwa bado mchanga… kimsingi
yeye ndiye aliyetuwekea dira na kujenga msingi tulioukuta sisi, bila
yeye tusingefika hapa tulipo.”
Nyuki wavuruga mazishi ya Saggaf
Waombolezaji waliofika kwenye mazishi ya Saggaf
walilazimika kukimbia kusaka hifadhi ya muda baada ya kundi kubwa la
nyuki kuvamia eneo la makaburi saa kumi jioni.
Mtu mmoja, ambaye inaelezwa alikuwa na tatizo la kutoona vizuri
alishambuliwa vikali na wadudu hao na kupelekwa Hospitali ya Regency kwa
matibabu.
Hali ilitulia baada ya saa moja hivi na kutoa fursa ya shughuli za maziko kuendelea.
Mtoto wa marehemu, Ahmed Saggaf alisema baba yake alifariki baada ya kulazwa kwa siku tano kutokana na matatizo ya figo na ini.
Ahmed alisema kisomo cha kumuombea marehemu kitafanyika leo katika Msikiti wa Kipwata, Kariakoo, Dar es Salaam.
Saggaf alikuwa Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM) kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Imeandikwa na Fidelis Butahe, Aidan Mhando, Elias Msuya na Joseph Zablon.
Akizungumza kwenye mkutano wa wafanyakazi na naibu
waziri huyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Vurugu alisema kitengo hicho
kimezidiwa na wingi wa maiti zinazopelekwa hospitalini hapo.
Alisema kitengo hicho cha kina majokofu sita tu na hulazimika kuhifadhi miili kwa zamu ili angalau maiti zisiharibike.
“Hata wewe Waziri ukifa leo, hakuna pa kukuweka.
Utawekwa sakafuni kusubiri maiti nyingine zipoe halafu utaingizwa ndani
kwa kuingizwa maiti mbili kwenye eneo la mtu mmoja,’’ alisema Vurugu.
Aliiomba Serikali ifanye haraka kuboresha kitengo hicho ili kuepusha tatizo la kuoza kwa miili ya marehemu.
Kumekuwa na malalamiko kuhusu uchache wa majokofu
ya kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo na baadhi ya watumishi
walisema hali kuwa mbaya zaidi inapotokea ajali ambayo inasababisha vifo
vya watu wengi kwa wakati mmoja.
Vurugu alidokeza pia kuwapo kwa tatizo katika
Idara ya Mifupa ya hospitali hiyo, akisema wakazi wengi wanaofika hapo
kwa matatizo hayo anawaona wakiondoka kwenda Hospitali za Peramiho ya
Ruvuma na Ikonda ya Makete huku wengine wakienda kwa waganga wa jadi
kuunga mifupa yao.
Vurugu alizungumza baada ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali
hiyo, Dk Humphrey Kiwelu kusoma taarifa ya utendaji mbele ya Naibu
Waziri iliyoonyesha hali iko shwari baada ya kudai kuwa hospitali hiyo
imepiga hatua kubwa kiutendaji na katika utoaji huduma kwa wagonjwa.
Dk Kiwelu alisema hospitali yake ina mafanikio
makubwa yakiwamo ya kuwa na maabara ambayo imekubalika katika kiwango
cha kimataifa na kwamba majibu yanayotoka kwenye maabara hiyo kwa sasa
yanakubalika hata Uingereza na Marekani.
Hata hivyo, alisema hospitali hiyo haina mashine ya CT Scan licha ya kuiomba kutoka serikalini tangu 2003.
Akijibu hoja mbalimbali za wafanyakazi, Dk Rashid
aliwataka viongozi kujipanga na kuchangua vipaumbele kutokana na
mafanikio mazuri yanayoonekana hospitalini hapo.
Alisema kwa kuwa hospitali hiyo imeongeza mapato
ya ndani kutoka Sh60 milioni hadi Sh300 milioni kwa mwezi, ipo haja ya
kutumia fedha hizo kuiboresha kwa kuangalia vitendea kazi zaidi na
masilahi ya watumishi wote.
Mwananchi
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment