
Muingereza David Cicil gerezani kwa madai ya tamthilia chafu
Uganda imepitisha muswada unaopinga mapenzi ya jinsia moja na
iwapo Rais Yoweri Museveni ataidhinisha sheria hiyo inamaanisha atakayepatikana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Muswada huo uliopitishwa na bunge
siku ya Ijumaa halikadhalika unasema mtu yeyote aliye na taarifa za watu
wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kushindwa kuripoti habari hizo
kwa maafisa wa polisi atafungwa gerezeni maisha.
Wakati huo huo bunge hilo hilo la Uganda siku ya Alhamisi liliidhinisha muswada unaopiga marufuku maonyesho ya picha chafu.
Mswada huo unaharamisha kitu chochote
kitakachoonyesha sehemu nyeti kama vile matiti, mapaja, makalio au tabia
yoyote inayozua uchu wa mapenzi.
Kulingana na mswada huo, sheria iliyopo sasa
kuhusu picha chafu haihusu zaidi picha hizo bali linahusu uchapishaji, mawasiliano, taarifa, burudani, maonyesho katika kumbi za kuigizia,
miziki inyochezwa katika vyombo vya habari, densi, sanaa, mitindo na
picha za runinga.
Mapema mwaka huu Waziri wa maadili wa Uganda,
Simon Lokodo, alipendekeza kuwa mwanamke yeyote anayevalia nguo ambayo
inafika juu ya magoti anatakiwa kukamtwa na kuadhibiwa kisheria.
Mswada huo unahitaji kuidhinishwa na Rais kabla ya kufanywa sheria.
Uganda ni nchi inayoshikilia mawazo ya
kihafidhina yaani isiyopendelea mageuzi katika mawazo na inaandaa sheria
ya kuwaadhibu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ikijumuisha hukumu ya
kifo katika baadhi ya kesi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment