Sejusa amemuonya Rais Museveni kuwa muda wake wa kutawala unakaribia ukingoni
Aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uganda UPDF,
Generali David Sejusa amezindua chama chake cha kisiasa nchini Uingereza
na kumuonya Rais Yoweri Museveni kuwa utawala wake wa miaka 28
unaelekea ukingoni.
Sejusa ambaye alikuwa jasusi wa zamani katika serikali ya Rais Museveni, amekiita chama chake "Freedom and Unity Front".
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda,
serikali ya Uganda imepuuza uzinduzi wa chama cha Sejusa huku msemaji
wa jeshi Paddy Ankunda akisema kuwa Sejusa anafamahu vyema kuwa amevunja
sheria kwani bado hajasataafu kutoka jeshini.
Wakati sejusa alipohojiwa kuhusu uzinduzi wa
chama chake, alisema kitaweza kuleta mageuzi. Alisema sio kwamba anataka
kufanya hivyo lakini ikiwa Rais Museveni ataendelea kuwatesa watu,
watafanya kila wawezalo kuweza kujilinda.
Mapema mwaka huu, generali huyo alitoroka Uganda
kutafuta hifadhi Uingereza baada ya kuandika barua iliyokuwa na madai
ya kutia wasiwasi mkubwa kuhusu serikali kupanga kuwaua wanajeshi wakuu
wanaopinga mipango ya Rais Museveni kukabidhi mamlaka kwa mwanawe
Brigedia Muhoozi Kainerugaba atakapoondoka mamlakani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment