Didier Drogba
Kitendo cha Didier Drogba na Emmanuel Eboue kuvua jezi na kuonesha ujumbe wa kumuenzi Mandela katika fulana zao kimewaingiza matatani. 

Tukio hili lilitokea mchezo ulipoisha baada ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya timu ya SB Elagizspor.

Drogba alivua jezi yake na kubaki na fulana  iliyokuwa na maneno yaliyosomeka "Asante Madiba; wakati Eboue katika fulana yake akimtukuza kwa ujumbe wa  "Pumnzika kwa Amani Nelson Mandela"”.

Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Uturuki (TFF) lilitafsiri tofauti tukio hilo na kuwataka Drogba na Eboue kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Wachezaji hawa walifanya tukio hili baada ya mchezo kuisha lakini wanaweza kufungiwa kwa kuwa TFF inakataza wachezaji kuonesha ujumbe wa kisiasa mchezoni.
Chanzo: Au.Sports
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top