Jack Patrick akiwa amefunikwa uso akiwa mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni.
MADAI ya kukamatwa kwa tuhuma za kumeza madawa ya kulevya aina ya Heroin nchini China kwa msanii, Video Queen na mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, kumeibua maswali ya kila aina, mengi yamesemwa, uvumi umeenea, lakini Ijumaa Wikienda linadondosha hatua kwa hatua.
Jack Patrick.
Baada ya kuinyaka taarifa hiyo ya aibu kwa staa huyo na taifa kwa
jumla, kwa uchungu mkubwa timu yetu imara ilijipanga na kuingia mtaa kwa
mtaa, nyumba kwa nyumba, mtu kwa mtu kuchimbua, kudadavua na kufukunyua
kwa undani zaidi juu ya tuhuma hizo. Aya zinazofuata zitakupa mwanga.
Wikienda lilichorewa mchoro kwamba, Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Macau nchini humo akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
Jack akiwa chini ya ulinzi.
Inadaiwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia kunaswa kwake ni uso wa uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria (passport) yake kuonesha kugongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara.
Habari zinasema ndipo maafisa wa uwanja huo walipomweka pembeni na
baadaye kumpeleka kwenye chombo cha kukagua kwa undani mwili wa
binadamu, walipojiridhisha ana ‘mzigo’ wakampa polisi mwanamke (WP) kwa
ajili ya kwenda kusimamia utoaji wa kete hizo chooni kwa njia ya haja
kubwa.
Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo Jack Patrick.
Baada ya kutoka chooni, ikafuata hatua nyingine. Jack aliwekwa mbele ya
mapaparazi akiwa amevalishwa maski nyeusi usoni ili asionekane sura
kisha akapigwa picha za kumwaga.
Sheria za Macau, mtuhumiwa huvalishwa maski usoni ili watu wasiione sura yake. Kete alizozitoa ziliwekwa juu ya meza, pia simu zake mbili, Iphone na Samsung nyeupe zilikuwa pembeni. Baadhi ya watu Bongo walizitambua simu hizo kwamba ni zake.
Jack ambaye ni Miss Ilala Namba
3, 2005, alikamatwa na madawa aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1
yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 kwa kuhifadhiwa ndani
ya kete 57.
Mwanamitindo Jack Patrick.
ATANYONGWA?
Kwa sheria za Beijing, China mtu akithibitika kubeba unga hukumu yake ni kunyongwa tu lakini waandishi wetu walipozungumza na wataalam mbalimbali wa sheria za kimataifa ili kujua ni adhabu gani inaweza kutolewa kwa mrembo huyo endapo atakutwa na hatia, walisema Beijing si Macau, ni vigumu kula kitanzi lakini kwenda jela miaka mitatu, minne au nane inaweza ikamhusu. Majimbo mengi ya China yanaongozwa kwa sheria zake badala ya sheria mama moja kwa nchi nzima.
Kwa sheria za Beijing, China mtu akithibitika kubeba unga hukumu yake ni kunyongwa tu lakini waandishi wetu walipozungumza na wataalam mbalimbali wa sheria za kimataifa ili kujua ni adhabu gani inaweza kutolewa kwa mrembo huyo endapo atakutwa na hatia, walisema Beijing si Macau, ni vigumu kula kitanzi lakini kwenda jela miaka mitatu, minne au nane inaweza ikamhusu. Majimbo mengi ya China yanaongozwa kwa sheria zake badala ya sheria mama moja kwa nchi nzima.
Hata hivyo, sheria za eneo alilokamatiwa zinasema kuwa uwezekano wa
ndugu, jamaa na marafiki kumuona kwa sasa haupo mpaka Machi, 2014
uchunguzi utakapokuwa umekamilika.
Wanahabari nchini China wakichukua picha za dawa za kulevya anazodaiwa kukutwa nazo Jack.
Awali,
baadhi ya watu wa karibu na modo huyo waligoma kuweka bayana kuhusu
yaliyompata Jack huko ughaibuni wakidai si wasemaje wake na kuwataka
mapaparazi kwenda kuchimba kwenye Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Kwa sharti la kutotajwa jina mahali popote kwenye ukurasa huu, mmoja
wa marafiki wa karibu wa Jack aliyeko China kwa masomo, alisema
amethibitisha ukweli kupitia balozi ndogo ya Tanzania nchini humo.
“Nilishituka sana niliposikia habari hizo, ikabidi nijiridhishe kwa kwenda kwenye ubalozi mdogo wa Tanzania nchini hapa na kupewa maelezo kamili juu ya sakata hilo.
“Nikaulizia uwezekano wa kuonana na Jack, nikaambiwa ni ngumu
kutokana na utata mkubwa juu ya ishu yenyewe,” alisema rafiki huyo na
kuongeza:
“Hata jana (Jumatano ya wiki iliyopita) gazeti moja liitwalo Daily China la huku lilitoa habari hiyo ndipo nikathibitisha baada ya kuona sura gazetini. Kweli ni Jack Patrick, najisikia uchungu na huruma juu yake, inauma lakini hatuna jinsi,” alisema rafiki huyo.
Kazi ni kazi tu. Timu
yetu ikiwa na kiu, hamu na shauku kubwa ya kuujua ukweli, ‘ilisaga lami’
mguu kwa mguu hadi kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Jack iliyopo
Mikocheni B jijini Dar ili kuona hali ikoje na kujiridhisha zaidi ambapo
iliashiria kila dalili ya kuwepo kwa habari mbaya.
Ukimya, utulivu na hali ya kupoa viliitawala nyumba hiyo baada ya
waandishi wetu kuwasili na kukuta hakuna chochote zaidi ya milio ya
ndege iliyokuwa ikisikika.
Mmoja wa waandishi wetu alipanda ukuta na kuchungulia ndani ambapo hakuona binadamu isipokuwa gari lake lile Benz jeusi likionekana liliegeshwa siku nyingi.
Roho za kutoridhika
ziliwasukuma mapaparazi wetu kuwatafuta majirani wa msanii huyo ili
kusikia walau chochote kipya kuhusiana na taarifa za Jack kunaswa na
unga.
“Mh! Hata sisi hatujui maana hatujamuona siku mbili hizi, lakini kama ni kusikia hata sisi tumesikia juu ya uvumi huo, lakini hatuna uhakika,” alisema mama mmoja (jina linavunda kwenye droo zetu).
Watu wengi (tukiwemo
sisi) wana hamu kubwa ya kujua ni nani hasa anahusika na mzigo ambao
msanii huyo anatuhumiwa kukamatwa nao. Katika pitapita ya waandishi wetu
kupeleleza kwa undani suala hili, lilibahatika kuzungumza na baadhi ya
watu ambao walihoji na kutaka kujua ni kigogo yupi yuko nyuma ya ishu
nzima.
“Lazima kutakuwa na mtu nyuma yake, si bure nyie fuatilieni sana,”
alisema mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe mahali popote.
Aliongeza kuwa, mtu anayekutwa na kete za unga tumboni maana yake katumwa (punda) na bosi wake, kwa hiyo suala kubwa kwa sasa ni kumsaka bosi huyo ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Hakuna ubishi
kwamba hali ni mbaya kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Kambarage jijini Dar, kwa madai kuwa piga, ua, galagaza mzigo
huo, Jack alikatiza nao pale.
“Jack alitokea Dar kwenda Thailand
kupitia Nairobi, lazima mzigo alitoka nao Bongo, tena jijini Dar. Sasa
pale eapoti alipitaje? Serikali iwachunguze wafanyakazi wa pale,”
alisema nguli mmoja wa filamu za Bongo (jina lake lipo).
Hii imekaa vibaya!
Wataalam mbalimbali wa masuala ya kisheria walizungumza na gazeti hili
juzi na kusema kuwa sakata la Jack ni kubwa zaidi ya lile la Agnes
Gerald ‘Masongange’ na nduguye, Melisa Edward waliokamatwa nchini
Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu.
Wakizungumza na Wikienda kwa
nyakati tofauti, baadhi ya wananchi walisema tukio la Jack limezidi
kuchagiza aibu kubwa kwa taifa katika medani za kimataifa kufuatia
matukio mengi ya Watanzania kukamatwa na madawa ya kulevya nje ya nchi.
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa
Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania,
Godfrey Nzowa alisema taarifa hizo zilimfikia kutoka kwa watu mbalimbali
wakiwemo waandishi wa habari, hivyo anaendelea kufuatilia suala hilo
kwa ukaribu zaidi ili kupata taarifa sahihi.
Aidha, Kamanda Nzowa alisema kuna wakati aliyekuwa mume wa
mwanamitindo huyo, Abdulatif Fundikira aliwahi kukamatwa na madawa za
kulevya nchini na kuachiwa kwa dhamana, ina maana kesi bado ipo
mahakamani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment