JESHI la polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia wanakijiji
zaidi ya kumi na tano (15) wakiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji,
mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Ntunduwalo, Afisa mtendaji wa
kijiji hicho na Afisa Mtendaji wa Kata ya Rwanda kufuatia wanakijiji
cha Ntunduwalo kuzuia magari yanayokwenda na kutoka yakiwa
yamesheheni Mkaa ya Mawe toka kwenye Mgodi wa Mngaka wilayani Mbinga
ambako polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
wakati wakizuia magari yaliyobeba makaa ya mawe mpaka walipwe fedha
za fidia wanazodai.
Habari zilizopatikana jana mchana Mjini Songea ambazo
zimezibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deudedit
Nsimeki zimesema kuwa tukio hilo lilianza kutokea juzi majira ya
saa za asubuhi ambako wananchi wa kijiji cha Ntunduwalo walijipanga
na kufunga barabara inayokwenda kwenye mgodi wa makaa ya mawe uliopo
karibu na kijiji hicho.
Alisema wanakijiji hao walikuwa na lengo la kuishinikiza
serikali ili iwalipe nyongeza ya fidia ambayo wanadai kuwa hapo awali
walipunjwa wakati wanafanyiwa tasmini ya mali zao zilizokuwepo ndani
ya maeneo yaliyochukuliwa na mgodi huo kwamba serikali ilitumia sheria
ya zamani badara ya sheria iliyopo hivi sasa ambayo inaonesha kuwa
ni kubwa.
Alifafanua kuwa kundi kubwa la wananchi wakiwemo watoto na
akina mama waliokuwa wamekaa mbele lililojipanga ni lile lililolipwa
mwanzo kwa kutumia sheria ya uthamini ya zamani ambapo wanadai kuwa
wamekuwa wakiahidiwa mara kwa mara na serikali kuwa watalipwa kiasi
cha fedha cha fidia kilichobaki.
Alieleza zaidi kuwa kutokana na hali hiyo wanakijiji hao waliamua
kuchukua uwamuzi wa kuzuia shughuli za magari yanayobeba makaa ya
mawe yasiingie kuchukua makaa ya mawe iwala kutoka kwenye eneo hilo.
Alibainisha zaidi kuwa kufuatia kuwepo kwa vurugu hiyo
iliyosababisha shughuli za mgodi kusimama polisi baada ya kupewa
taarifa hiyo walikwenda kwenye kijiji hicho wakiwa wameongozana na
katibu tawaa wa wilaya ya Mbinga Idd Mponda ili kujaribu kuongea na
wananchi, kuwasii waondoe kizuizi hicho ili magari yaendelee na kazi
ya kusomba makaa yam awe lakini wananchi walikataa na walimueleza
katibu tawala huyo kuwa hawamuitaji kumuona yeye pamoja na watu wengine
wala Mkuu wa wilaya hiyo kuwasikiliza wanachotaka walipwe fedha
zao wanazodai na si vinginevyo.
Aliongeza kusema kuwa mvutano huo wa mazungumzo kati ya katibu
tawala wa wilaya hiyo Mponda na wanakijiji yalidumu kwa muda mrefu
hadi juzi majira ya saa tatu usiku polisi waliamua kulilinda eneo
hilo na baadaye walifanikiwa kuwakamata watu watano ambao wanadaiwa
kuwa ndio waliokuwa viongozi wa vurugu hizo.
Amewataja baadhi ya wanashikiliwa kuwa ni Mwenyekiti wa serikali
ya kijiji cha Ntunduwalo John Nyimbo (36), Matrida Nchimbi ( 49)
ambaye ni Afisa mtendaji wa kata ya Rwanda, Joachim Ngaponda ambaye ni
Afisa mtendaji wa kijiji hicho, mwenyekiti wa kamati ya miradi ya
kijiji hicho Garusi Komba (49) na John Joachim Mahai (45) mkazi wa
kijiji cha Malindindo tarafa ya Mbuji wote wanaendelea kuhojiwa na
Polisi.
Aidha, Kamanda Nsimeki alisema kuwa pamoja na polisi
kuwashikiria wanakijiji hao jana majira ya asubuhi vurugu
zilirejea tena ambapo polisi walilazimika kutumia mabomu ya
machozi kuwatawanya wanakijiji hao ambao waliendelea kuyazuia
magari yaliyokuwa yamebeba makaa ya mawe huku wananchi wakijitahidi
kuyazuia yasipite.
Hata hivyo jitihada za songeayetu kumpata mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya Mbinga ambaye pia ni mkuu wa wilaya
hiyo Senyi Ngaga ziligonga mwamba baada ya kupigiwa simu kwa
zaidi ya mara tatu ambayo haikuweza kupokelewa na baadaye alipopigiwa
simu mara ya nne ilipokelewa na mtu mwingine ambaye alidai kuwa DC
yupo kwenye kikao hivyo hana nafasi ya kuongea muda huo.
0 comments:
Post a Comment