Wanajeshi wa RENAMO wakiwa na silaha
Zimbabwe imewatahadharisha wanaharakati wa RENAMO nchini Musimbiji kutoanzisha mapigano baada ya kujiondoa katika mazungumzo ya amani ya 1992.

Naibu Waziri wa masuala ya kigeni wa Zimbabwe Christopher Mutsvangwa ameiambia BBC kuwa hawatavumilia kuona vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vilivyowahi kutokea nchini humo.

Mawazo ya kundi la wanaharakati wa RENAMO yalisababisha kuvunjika kwa mazungumzo ya amani ya 1992 ambapo waliazimia kuwa na takriban wapiganaji 1000 na wabunge 51.

Katika onyo hilo Mutsvangwa amesema Renamo wanapaswa kuungana na mchakato wa kisiasa na kuachana na kuchochea mapigano hali itakayoleta dosari katika ukanda.

Mutsvangwa amesema SADC haitavumilia kuona RENAMO ikianzisha machafuko kama mapiagano ya wenyewe kwa wenyewe ya mwaka 1976 hadi 1992 yaliyosababisha kiasi cha watu million moja kuuawa.

RENAMO imejiondoa katika mazungumzo baada ya serikali ya Msumbiji kutoa amri ya kutaka kuidhibiti ngome ya Dhlakama katika milima ya Gorongosa kati kati mwa Msumbiji wakimtaka kiongozi huyo kuondoka.

Tishio hilo la kundi la RENAMO kuanzisha mapigano linakuja wakati ambapo Msumbiji imepata ongezeko la kiuchumi baada ya kugunduliwa kwa gesi mwaka 2011 hali iliyochochea uchumi.

Msuluhishi wa Msumbiji Lourenco do Rosario amesema kuwa amekuwa na mazungumzo na na waasi hao ili kurejesha hali ya utulivu.

Pamoja na msimamo huo wa Renamo kujitoa lakini bado wabunge wake 51 bado hawajatangaza kujitoa katika bunge huku RENAMO pia wakidai serikali ya nchi hiyo imeshindwa kuweka mazingira huru na haki ya uchaguzi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top