KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa
Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka
(16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa
kung’atwa ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje,
kama ambavyo anaonekana pichani ukurasa wa mbele.
Tukio
hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa
hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi
kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.
Tunaweza
kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance
Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita.
Akizungumza
na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya
kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Aliliambia
Majira kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba
koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema
akitoa ulimi nje.
DC
Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa mbwa na
kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na
maumivu.Aliongeza
kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.
“Unaweza kusema kuwa
ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula
ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana
na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea
kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza
kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la kuchoma.
“Mshtakiwa huyo
alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza vipande
vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC Mwamotto wakati wa
mahojiano na Majira.
Baada ya kumaliza
kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza
na vipande.
Alisema kuwa wakati
anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba
msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena kipande cha mdomo wa chini
na kisha kusababisha meno kubaki nje.“Kutokana na kelele
hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini walikuta tayari, Susuluka
amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka kwa wingi,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa
kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na kumpeleka katika Kituo
cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya
Kibondo.
Majira iliendelea
na mahojiano hayo ambapo, mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya
na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili.“Hivi sasa mshtakiwa
yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha kusikitisha tena akiwa huko
alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu mshtakiwa mwenzake,” alisema.
Alisema kuwa
mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali
iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi nimelazimika
kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa huyu, kwani hili tukio
linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa
gani ya kuua mbwa au kumng’ata mtu,” alisema.
Alisema kuwa pia
amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika
hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada
kutoka Wizara ya Afya ili mgonjwa huyu akatibiwe India na tayari maandalizi
yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa
mgonjwa huyo hana pua, macho yamefumba, mdomo kwa kujeruhiwa vibaya usoni hali
ambayo anahitaji matibabu zaidi.Amewaomba Watanzania kumsaidia kijana huyo ili aweze kwenda
kutibiwa haraka nje pamoja na kupata msaada mbalimbali kwa kuwasiliana na
mganga mkuu wa hospitali ya Kibondo ama kuwasiliana na Mhariri mtendaji wa
gazeti hili la Majira
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment