Naibu rais wa Kenya William Ruto
Wabunge nchini Kenya wanatarajiwa kukutana kwa dharura hii leo kujadili ikiwa nchi hiyo itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC au la.

Hatua hii ya wabunge inakuja zaidi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya naibu Rais wa Kenya Williiam Ruto kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2008.

Ruto anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwa kufika katika mahakama hiyo mwezi Novemba kwa kesi dhidi yake.
Wawili hao wanashtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2007.

Msemaji wa ICC ameambia BBC kuwa kesi hiyo itaendelea hata ikiwa Kenya itajiondoa kwenye mkataba wa Roma uliopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Bwana Fadi El Abdallah, alisema kuwa itachukua karibu mwaka mmoja kwa mchakato wa nchi yoyote yoyote ile kujiondoa kutoka katika mahakama ya ICC na hii bila shaka inaathiri tu kesi zilizokuwa mbele ya mahakama hiyo kwa wakati huo.

Hii ni hatua ya dharura inayochukua serikali kujitoa katika Mkataba wa Roma wa mahakama hiyo ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa mnamo tarehe 17 July, mwaka1998.

Kenya inataka kutoa mfano wa kuwa nchi ya kwanza Afrika kuchukua hatua hiyo licha ya kwamba uamuzi huu hautoathiri kwa namna yoyote kesi zinazoendelea sasa katika mahakama ya ICC.

Mahakama hiyo ya kimataifa imesema kwamba kesi hizo zitaendelea hata iwapo Kenya itajitoa.

Imesema itaichukua Kenya kiasi ya mwaka mmoja kabla ya kukubaliwa ombi hilo la kutaka kujiondoa katika mkataba wa Roma na hilo litaathiri tu kesi zitakazozuka baada ya muda huo.

Haya yanajiri wakati makamu wa rais William Ruto anatarajiwa kuondoka Kenya kueleka Hague Uholanzi wiki ijayo kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadaamu katika mahakama hiyo ya ICC, kesi inayoanza tarehe 10 mwezi huu.

Wote wameshtakiwa kwa kuhusika katika ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.Kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza tarehe 12 mwezi Novemba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top