Viongozi wa mataifa wanachama wa kundi la G20
wanakusanyika katika mji wa St Petersburg nchini Urusi kwa mkutano wao
wa kila mwaka wa mataifa ishirini yenye ustawi mkubwa wa kiviwanda
duniani.
Duru zinasema maswala ya kiuchumi huenda
yakafumbiwa macho katika mkutano huo kutokana na mzozo uliopo nchini
Syria na tofauti zilizopo kati ya Marekani na Urusi kuhusu mipango ya
kuishambulia Syria kwa madai ya kutumia silaha za kemikali.
Rais Barack Obama anasema kuwa dunia haiwezi kuepuka tendo la kutochukua hatua dhidi ya Serikali ya Syria.
Naye Rais Vladimir Putin amesema kuwa Marekani
ikishambulia Syria litakuwa tendo la uchokozi. Rais wa Marekani ameeleza
kwamba Serikali ya Syria imekaidi marufuku ya kimataifa ya kutumia
silaha za kemikali na hatua inapaswa kuchukuliwa.
Kiongozi wa Urusi anasema vingine kuwa Marekani
kushambulia Syria bila idhini ya Umoja wa Mataifa ni kukiuka sheria ya
kimataifa.
Hapa hali ya maoni mawili yanayohitiliafiana kutoka kwa Marais wawili maarufu.
Inaonekana kuwa tofauti kubwa inayohusu Syria
huenda ikapata nafasi bora katika vyombo vya habari kuliko mkutano
unaoendelea wa mataifa tajiri zaidi duniani ya G20. Marais hawa wawili
ni wanachama wa G20 ambapo watataka kushawishi mataifa kuunga mkono
upande wao.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment