Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) linasema kuwa
zaidi ya watu milioni mbili nchini Zimbabwe wanakabiliwa na tishio la
njaa katika miezi michache ijayo.
Shirika hilo la WFP, linasema kuwa mtu mmoja kati ya watu wanne katika maeneo ya vijijini wanahitaji msaada wa chakula.
Idadi hii ya watu wanaohitaji msaada
inasemekana kuwa kubwa zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 2009 wakati ambapo
zaidi ya nusu ya wananchi walihitaji msaada kama huo.
Tatizo hilo ni baya zaidi Kusini mwa Zimbabwe ambako mavuno hayakuwa mazuri mwaka huu.
WFP linasema kuwa tisho la uhaba wa chakula
limesababishwa na hali mbaya ya anga, bei ghali ya nafaka na ukosefu wa
mbegu za hali ya juu, mbolea na mahitaji mengine ya kilimo bora.
Ili kukabiliana na hali nchini Zimbabwe, shirika
la WFP na washirika wake linatarajia kutoa nafaka, mafuta na mboga kwa
watakaokabiliwa na hali mbaya zaidi.
Mnamo mwaka 2012, kwa mara ya kwanza serikali ya
Zimbabwe ilitoa mbegu za thamani ya dola milioni 10 kwa wakulima
kutokana na mradi walioshirikiana nao na shirika la WFP na washirika
wake wengine kwa wilaya 37.
Ili Kuwasaidia watu kukabiliana na njaa, shirika
la WFP limekuwa likiendesha mpango wa kuwapa watu pesa badala ya
chakula katika maeneo ya vijijini tangu mwezi Juni.
Chini ya mpango huu jamii ambazo zinakabiliwa na
tisho kubwa zaidi hupokea chakula au pesa wakati wakijihusisha na
miradi ya kusaidia jamii kama vile ujenzi wa mabwawa.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment