Vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema viko katika
mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo zima la Westgate ambapo hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote wameokolewa huku wanamgambo
sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisa
Duru kutoka shirika la AFP zinasema
kuwa majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili
ambao wamesalia ndani ya jengo la Westgate.
Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa
ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya
juu zaidi ya jengo hilo.
Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka katika jengo hilo.
Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya
Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa
kwa siku ya nne.
Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.
17:19 Mwandishi wa Nation TV Larry Madowo
KUPITIATwitteranasema :Karibu wanajeshi kumi na wawili wako kwenye paa
la jengo la Westgate wakishika. Anauliza je shughuli ya kuwasaka magaidi
imekamilika?
17:15 Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa
wananchi walioyaacha magari yao katika jengo hilo wametakiwa na maafisa
wa usalama kwenda kuyachukua, ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa.
17:14 Milio ya risasi ilisikika mchana huu huku
majeshi ya Kenya yakiendelea kukabiliana na magaidi waliosalia ndani ya
jengo la Westgate. Mapema serilali ilisema kuwa magaidi sita waliuawa
usiku wa kumkia leo na wengine hapo jana.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment