Na Gideon
Mwakanosya,Songea
WAANDISHI wa habari
wawili wawakilishi wa vyombo vya habari tofauti mkoani Ruvuma wamefukuzwa
kawenye ziara ya waziri mkuu wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mizengo Pinda kwa kushutumiwa kuandika habari ya ajali iliyotokea kwenye ziara
hiyo wakati msafara wa waziri mkuu ukitoka wilayani Tunduru kuelekea wilyani
Namtumbo.
Habari zilizopatikana
jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na katibu wa chama cha waandishi wa
habari wa mkoa wa Ruvuma Andrew Chatwanga zimeeleza kuwa tukio la kufukuzwa kwa
waanahabari hao wawili limetokea jana majira ya saa 1.45 katika eneo la Ikulu
ndogo ya mjini Songea wakati msafara huo unatarajia kuondoka kuelekea wilayani Nyasa.
Baadhi ya mashuhuda wa
tukio hilo wakiwemo waandishi wa habari wa mkoani Ruvuma ambao walionyesha
kushangazwa na tukio hilo la mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu Said
Nguba kuwahoji kwa nyakati tofauti wanahabari hao wawili kuhusiana na tukio la
ajali iliyotokea juzi kwenye ziara hiyo ya waziri mkuu ambayo ilisababisha
magari manne kugongana na kusababisha taharuki kwenye msafara huo huku baadhi
yao kujeruhiwa.
Walisema kuwa mara baada
ya ajali hiyo kutokea kulitolewa maelekezo na Afisa habari wa mkoa wa Ruvuma
Revokatus Ksimba mbele ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la tukio
kuwa taaifa hiyo ya ajali isitangazwe kwenye vyombo vya habari kwa madai
kuwa haina madhara makubwa kauli ambayo ilipingwa pale pale na baadhi ya waandishi
wa habari .
Ajali hiyo
ilihusisha magari manne yenye namba za usajili PT 1437 Mali ya jesji la
polisi,STK 7929,DFP 6627 na DFP 8709 iliyokuwa imewabeba baadhi ya waandishi wa
mkoa wa Ruvuma pamoja na Afisa habari wa mkoa huo ambaye anadaiwa kuwa alipewa
maelekezo na baadhi ya waandishi wa habari waliotoka jijini Dar Es Salaam
pamoja na mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu ambao walitoa maelekezo
kuwa ajali hiyo ni ndogo na haina haja kuandikwa na kutangazwa kwenye vyombo
vya habari jambo ambalo baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma
walilipinga kwa sababu wao ndiyo wahanga.
Katika ajali hiyo jumla
ya waandishi habari nane wa mkoani Ruvuma walikuwemo kwenye magari mawili kati
ya magari manne yaliyopata ajali hiyo iliyotokea kwenye kijiji cha Namingwea
wilayani Namtumbo kwenye msafara huo.
Hata hivyo katibu wa
chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma Chatwanga alionyesha kusitikishwa
na kitendo cha kuwafukuza waandishi wawili ambao ni Nathan Mtega mwakilishi wa
ITV na Radio One Stereo mkoani Ruvuma na Ngaiwona Nkondola mwakilishi RFA na
STAR TV Mkoani Ruvuma ambao wanadaiwa kuandika na kutangaza habari za tukio
hilo la ajali iliyotokea wakati wao kama wanataaluma wa tasnia ya habari
wamehabarisha jamii yaliyojiri kwenye msafara huo.
Hata hivyo jitihada za
kumpata mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu Nguba zimeshindikana kwa
kuwa bado yuko kwenye msafara huo wa waziri mkuu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment