Wakati uamuzi huo ukitolewa na Jaji Lukelelwa,
washtakiwa wote watano wa kesi hiyo, Henry John Kileo, Evodius Justian,
Oscar Kaijage, Seif Kabuta na Rajab Kihawa hawakuwa katika chumba cha
mahakama muda wa saa tatu na nusu asubuhi.
Washtakiwa walifikishwa mahakamani hapo majira ya
saa nne na dakika arobaini na waliarifiwa na wakili mwakilishi, Emanuel
Msyani kuwa shauri limepangwa tarehe tano mwezi ujao wakiwa ndani ya
chumba cha mahabusu ya Mahakama Kuu.
Wakili Msyami alisema Mahakama Kuu iliridhia ombi
la upande wa Jamhuri kuomba kuongezewa muda angalau kwa siku moja kwa
vile walipokea hoja Ijumaa iliyopita.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na
kuongeza muda hadi tarehe moja uwe umewasilisha majibu ya hoja na
kuipanga tarehe tano kwa ajili ya uamuzi.
Kesi hiyo ya rufaa ya jinai namba 53/2012
ilifunguliwa na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala na kuanza kusikilizwa
Julai 22 mwaka huu mbele ya Jaji Lukelelwa ikiomba miongozo ya kisheria
ikiwemo yaliyotolewa na mahakama za wilaya na mkoa.
Shauri la maombi ya marejeo liliwakilishwa na
Wakili Peter Kibatala anayewatetea washitakiwa, akiiomba mahakama kuu
ipitie majalada ya kesi mbili dhidi ya wateja wake zilizofunguliwa
mahakama hizo baada ya kuona maamuzi yake hayakutenda haki.
Wakili Kibatala alibainisha katika maombi hayo
kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki
za waomba rufaa ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki ya kupata dhamana.
Kwa upande wake Serikali ilishindwa kujibu maombi
hayo, badala yake ilijenga hoja kwamba walichelewa kupata nyaraka hizo
kwani walizipokea siku moja kabla ya kutajwa shauri hilo hivyo
walishinda kuzijibu.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment