Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dare Salaam Profesa Rwekaza Mukandala

Chuo  kikuu cha Dar es Salaam UDSM kinataraji kuanza kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza inayohusiana na mafuta na gesi asilia kuanzia mwezi oktoba mwaka huu.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam  kimesaini mkataba wa makubaliano ya kutoa mafunzo hayo na kampuni ya General Electrical Company ya Marekani.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala amesema kuwa kuanzia mwezi oktoba mwaka huu chuo kitaanza mafunzo kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014 unaotaraji oktoba mwaka huu.

Hapo awali haikuwepo kozi ya aina hiyo hapa nchini
Naibu Makamu mkuu wa chuo anayeshughulikia fedha na utawala, Profesa Yunus Mgaya, amesema usimamizi wa masuala ya gesi unahitaji utaalam na umakini  mkubwa hivyo kuanzishwa kwa kozi hiyo kutainufaisha Tanzania  kupata wataalam wengi katika masuala ya mafuta na gesi asilia.

Profesa Mgaya amesema chuo chake kwa kushirikiana na wataaalam wa sheria na nchi ya china wameandaa mitaala itakayowezesha mafunzo ya utafiti,usimamizi, uchimbaji usafirishaji hata matumizi ya nishati hizo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

1 comments:

Anonymous said... June 22, 2013 at 8:54 AM

mmbona dom ipo ya petrol

 
Top