Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameweka bayana kuwa wanaunga
mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na
Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama
chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai
kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati
kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa
sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani
wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe
alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa.
Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa
na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na
uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo.
Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi
ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa
sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila
upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha
nyingi kwa kazi kidogo yatakoma.”
Msimamo wa Sumaye
Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.
Sumaye alisema muungano wa Serikali tatu haufai akisema utasababisha mvutano mkubwa wa kimadaraka na rasilimali.
Sumaye anaungana na wanasiasa wengine waliopinga
muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
wengine wakiwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel
Sitta, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Mbunge wa
Urambo Magharibi (CCM) Profesa Juma Kapuya, Mbunge wa Kigoma Mjini
(CCM), Peter Serukamba na Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano na
Uchukuzi, Dk Maua Daftari.
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dira
ya Dunia kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC),
akiwa Johannesburg, Afrika Kusini mwishoni mwa wiki, alisema Serikali
tatu zinaweza kutikisa Muungano.
“Huwezi kutatua matatizo kwa Serikali tatu...
unaweza kuyaongeza kwani kutakuwa na Serikali tatu na marais watatu...
kama kuna mvutano baina ya Serikali mbili ukiongeza ya tatu inaweza kuwa
na mvutano zaidi,” alisema na kuongeza:
Profesa Lipumba alisema hakuna mantiki ya kupiga kura ya maoni
ya Katiba ya Muungano bila kuwa na Katiba ya Tanzania Bara na
marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Profesa Lipumba alisema mapendekezo ya msingi ya CUF ni kwamba,
kura ya maoni isubiri kukamilishwa kwa rasimu ya Katiba ya Tanzania Bara
na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar.
Alisema licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
kufanya kazi nzuri ya kuratibu maoni bila kushinikizwa na matakwa ya
CCM, kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo yameachwa kwenye rasimu.
“Huwezi kuacha vitu kama umilikaji wa ardhi,
maliasili na rasilimali za nchi, elimu, afya na mazingira ya kukuza
uchumi na uhuru wa Serikali za mitaa. Rasimu imeshughulikia mambo ya
Muungano.”
“Maoni ambayo CUF tuliyatoa ikiwamo muundo wa
Serikali tatu, kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, Rais kutangazwa baada ya
kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, Spika kutokuwa mbunge na
mengineyo yamepata nafasi.”
Mwananchi
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment