Zitto Zuberi Kabwe
Kesho
jumamosi wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya Gesi Asilia.
Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo.
Ikumbukwe kwamba kuanzia tarehe 22 - 23 Mei 2013 kutakuwa na mjadala wa
bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Semina hii Ni maandalizi ya
Bajeti hii.
Jambo la kushangaza ni kwamba wakati sera ya Gesi Asilia ipo
kwenye rasimu na ndio kwanza wabunge tumeletewa
kutoa maoni, Serikali tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya Mafuta
na Gesi kwenye Bahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.
Zabuni hii mpya
ya vitalu vya utafutaji imetolewa wakati kuna maamuzi ya Bunge kuzuia
ugawaji huu mpya mpaka sera ya Gesi Asilia na Sheria ya Gesi vikamilike.
Haraka hii ya serikali kugawa vitalu bila sera wala sheria inatoka
wapi? Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na
kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa Kwa vizazi vya sasa
na vijavyo.
Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo kwa sera
na sheria mpya unapaswa kupingwa kwa Nguvu zote.
Tafuta mbunge wako,
mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali.
Tumalize kwanza sera na
Sheria ndio tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment