Mizengo Pinda. |
Serikali
imeahidi kuwajibisha watendaji watakaobainika kwenda kinyume katika
uingizaji wa mfumo mpya wa usahihishaji mtihani wa Kidato cha Nne mwaka
2012, ambao matokeo yake yamefutwa.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Tume hiyo haijakamilisha kazi yake, lakini muda si mrefu itakuwa imekamilisha na kuwasilisha maelezo ya kina yatakayoipa Serikali majibu kwa maeneo yote.
“Tusubiri kidogo, muda
si mrefu tutakuwa tumekamilisha kazi …na kama wapo watu waliosababisha
jambo hili, wala haitakuwa tatizo hata kidogo kuchukua hatua za
kuwawajibisha. Ni dhahiri kwamba suala hili si dogo,” alisema Waziri
Mkuu.
Majibu hayo ya Pinda yalitokana na maswali ya Mbunge Sakaya,
ambaye alisema uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo hayo kutokana na
kubainika kulikuwa na mabadiliko ya upangaji wa alama bila kuandaa
wanafunzi, si jambo dogo.
Sakaya ambaye alitaka kusikia kauli ya Serikali, alihoji, “Hili si jambo dogo, ni kubwa sana. Elimu ni kitovu cha maendeleo ya taifa lolote, haiwezekani utaratibu mpya
ukaingizwa kwenye mfumo bila kushirikisha wadau wakiwemo maofisa elimu na walimu.
Akimjibu,
Waziri Mkuu alisema Tume inaendelea kukamilisha kazi yake, ili kuja na
maelezo fasaha juu ya nini kimetokea, na athari zilizojitokeza kutokana
na hatua hiyo ya matokeo mabaya.
Hata hivyo Sakaya aliendelea kusema matokeo yameleta madhara makubwa kwa jamii, ikiwemo watoto waliopoteza maisha, wengine kukimbia familia zao na baadhi ya wazazi kufedheheka na kupata presha.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, huoni umuhimu wa kuwajibisha
watendaji wote waliohusika wakianzia na Waziri mhusika wa wizara hii
(Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa) ambaye
aliruhusu mfumo huo?” Alihoji Sakaya.
Waziri Mkuu pamoja na kujibu
kwamba haitakuwa tatizo kuchukua hatua za kuwawajibisha watendaji
husika, alisisitiza baada ya kazi ya Tume, Serikali itapata maelezo ya
kina na majibu kwa maeneo yote.
Mwezi uliopita, Serikali ilitoa
taarifa bungeni juu ya uamuzi wa kufuta matokeo ya mtihani wa kidato
cha nne, uliofanyika mwaka jana na kutangazwa Februari mwaka huu.
Taarifa hiyo, ilitolewa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu taarifa ya awali ya Tume ya Taifa ya kuchunguza matokeo hayo, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Pinda kutokana na matokeo kushuka kwa kiwango kikubwa.
Taarifa hiyo, ilitolewa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu taarifa ya awali ya Tume ya Taifa ya kuchunguza matokeo hayo, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Pinda kutokana na matokeo kushuka kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa Lukuvi, Baraza la Mawaziri liliridhia mapendekezo ya Tume hiyo na kutaka yatekelezwe mara moja. Ilielezwa mfumo uliotumika mwaka jana katika kupanga matokeo na madaraja, ulikuwa tofauti na uliotumika mwaka juzi na miaka iliyotangulia.
Matokeo
yaliyotangazwa Februari 2012 yalionesha kati ya wanafunzi 367,756
waliofanya mtihani huo, watahiniwa 126,847 ndio waliofaulu. Kati ya hao,
waliofaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ni 23,520 sawa na
asilimia 6.4 na daraja la nne ni 103,327 sawa na asilimia 28.1 huku
watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 ya wanafunzi wote walipata
sifuri.
Tume ya Uchunguzi inayotarajiwa kukamilisha maelezo yake hivi karibuni, ilipewa hadidu za rejea ambazo ni kubainisha sababu za matokeo hayo mabaya, kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua.
Hadidu nyingine za rejea ni
kutathmini nafasi ya halmashauri katika kusimamia elimu ya sekondari
katika halmashauri zake na kuainisha sababu nyingine zinazoweza kuwa
zimechangia hali hiyo ya matokeo.
0 comments:
Post a Comment