Sheikh wa  mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amelaani tukio la kushambuliwa kwa waumini waliokuwa wakisali katika kanisa la Mtakatifu Joseph jimbo kuu la Arusha ambalo limegharimu maisha na watu zaidi ya 60 kujeruhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo Kiongozi huyo amesema tukio hilo linasikitisha  na linatakiwa kulaaniwa na  kila mpenda amani kwani vitendo kama hivyo havikubaliki katika jamii.

Sheikh Mussa Salum amewataka watanzania kujiepusha na wananchi ambao kwa sababu za maslahi yao binafsi wanataka kuivuruga amani ya Tanzania kwa itikadi za kidini.

Aidha katika hatua nyingine kiongozi huyo amewatahadharisha watanzania  kutoyanyooshea makundi au madhehebu mengine ya kidini kuwa yanahusika katika shambulio hilo.

Sheikh Alhad Mussa Salum ameshauri suala hilo liachwe mikononi mwa vyombo vya usalama kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini ukweli wa tukio lenyewe.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top