Habari kutoka Iringa zinasema kuwa kuna vurugu zinaendelea kati ya wamachinga na jeshi la polisi ambapo mabomu yanapigwa ili kuzuia maandamano eneo la Mashinetatu katika Manispaa ya Iringa.

Chanzo cha vurugu hizo inasemekana ni wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga kutaka kufanya maandamano kupinga kuzuiwa kufanya biashara katika eneo la mashinetatu lililo katikati ya mji.

Jeshi la polisi halitaki kuona mkusanyiko wowote ule na pindi linapobaini maji ya kuwasha au mabomu ya machozi yanatumika kuwatawanya watu.

Hata hivyo, kazi inakuwa ngumu kwa vile wamachinga inasemekana wanahama kutoka eneo moja hadi lingine wakiwa katika vikundi vidogo.

Habari zinaeleza zaidi kuwa watu waliokuwa wanaenda ibadani, wengine kwenda kupata mahitaji ya kawaida na hata wale waliokuwa wanataka kufuatilia kinachoendelea kwa vile hawakuwa na habari, baadhi yao wameishia kurushiwa maji ya kuwasha au kupigwa mabomu ya machozi.


 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top