Serikali imesema ujenzi wa viwanda katika mikoa ya Lindi na Mtwara utasaidia kukuza shughuli za maendeleo  ya  shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter  Muhongo amesema kuwa kuanzishwa na kujengwa kwa  bomba la gesi asili nchini ni faida badala ya kutumia  mafuta ya taa na mkaa.


Akizungumza  wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo ya nishati na madini Prof. Muhongo amesema kuanzishwa kwa mradi  wa gesi asilia  kutasaidia kukuza pato la taifa .


Hata hivyo  kambi lasmi ya upinzani kupitia  Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA Mh.John Mnyika , ameiomba serikali iahilishe utandazwaji wa bomba la gesi asili ili wananchi waelimishwe  na kuhakikisha mikataba yote  juu ya gesi na iwekwe wazi kwa wananchi ili kuepusha vurugu.


Wakati wa bajeti hiyo ya wizara ya nishati na madini ikiwekwa mezani mambo kadhaa yanatarajia kuibuliwa katika miradi ya gesi asilia  ikiwa ni pamoja na kuanzishwa  kwa viwanda, kuongezeka kwa ajira pamoja na kukua kwa uchumi wa nchi.


Hivi karibuni wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waliandamana wakipinga kujengwa kwa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, kitu kilichofafanuliwa na waziri Mhongo kama ni changamoto ambayo yaweza kukwamisha mchakato wa kutekeleza miradi ya maendeleo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top