Na Gideon Mwakanosya,Songea.
ASKARI wa Kampuni binafsi ya ulinzi ya Kasamwa Security Guard Faraja Mapunda mwenye umri kati ya miaka 60 na 65 amekutwa amekufa akiwa kazini huku amebeba bunduki kwenye lindo lililopo mtaa wa Zanzibar katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki zimesema kuwa tukio hilo limetokea mei 27 mwaka huu majira ya saa 9 usiku huko katika mtaa wa Zanzibar katikati ya manispaa ya Songea.
Alisema kuwa siku hiyo ya tukio Mapunda akiwa kazini kwenye lindo alilokuwa amepangiwa na mwajiri wake pamoja na mlinzi mwenzake Asha Ponera (37) ghafla alianguka na kufa papohapo.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kutokea tukio hilo Asha ambaye ni mlinzi mwenzake aliwasiliana na mwajiri wake kumjulisha juu ya tukio hilo ambapo baadae mwajiri wake alifika kwenye eneo la tukio na kuchukuwa hatua ya kuwasiliana na jeshi la polisi ambapo askari wakiwa wameongozana na mganga walifika kwenye eneo la tukio na kumkuta mapunda tayarai amekwisha kufa.
Kamanda Nsimeki alisema kuwa kwa hivi sasa mwili wa marehemu Mapunda umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi mahiti cha hospitali ya Mkoa (HOMSO) kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
MWISHO.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment