Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini kasoro
iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa
maadili.
FIFA
ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu
mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya
wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013,
lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji wa
vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa
TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa
shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya
Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013 na maamuzi yake kutumwa
juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa FIFA, Jerome Valcke.
Baada
ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana kukutana
na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT).
“Matarajio
yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye uchaguzi.
Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa hili ni jambo la
kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia itaonekana imetendeka.” alisema
Tenga, ambaye alishatangaza kuwa hatagombea tena urais baada ya kuliongoza
Shirikisho kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja.
“Lengo
letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika mapema
iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza kufanyika kwa
pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na
FIFA.”
Uchaguzi
wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa ukielekea
ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua ya mwisho na
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika barua FIFA kuomba
iingilie kati.
Rais
Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote zilizoathiriwa na
mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya taarifa hizo, maagizohayo ya
FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo ya muda mrefu katika uendeshaji wa
mpira wa miguu nchini.
Katika
barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1.
Kuunda
vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo ni cha
kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake yatakuwa ni
kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2.
Kufanya
mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3.
Kuanza
upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua milango kwa
wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4.
Shughuli
hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika
kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa ajili ya
kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za maadili na
Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati
Mpya ya Utendaji.
Katika
maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya TFF
iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa walikiuka Ibara ya
9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya Katiba ya TFF ambavyo
vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani, kufuja fedha za shirikisho na
ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata
hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na kamati husika
(kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za uchaguzi za TFF.
“Kutokana
na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa akienguliwa
kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni ya muda gani,”
inasema barua hiyo ya FIFA.
Rais
Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF
kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa lengo la
kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema iwezekanavyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment