Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemwandikia Spika wa Bunge barua ikimtaka Waziri wa Nishati na Madini aeleze sababu za kutoa leseni ya uchimbaji Uranium Wilayani Namtumbo kinyume na sheria.
Yafuatayo ni maelezo ya Mheshimiwa Zitto yaliyopatikana katika ukurasa wake wa facebook
Nimeandika
barua Kwa Spika wa Bunge kutaka Waziri wa Nishati na Madini kutoa
maelezo Bungeni kuhusu uamuzi wake wa kuwapa leseni kubwa ya kuchimba Uranium huko wilayani Namtumbo. Mnamo tarehe 10 Agosti 2012 Waziri
alitamka ndani ya Bunge "sisi tunajua zaidi ya anavyojua yeye, Leseni
haijatolewa na haitatolewa mpaka Kampuni ya Mantra Resources ilipe
kodi".
Kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) ya $189m kufuatia
mauzo ya mradi wa #Mkuju River Project kutoka kampuni ya Mantra kwenda
kampuni ya AMRZ ya Urusi iligomewa kulipwa.
TRA wamepeleka shauri hilo
mahakama ya kodi na mpaka sasa maamuzi hayajatolewa.
Kwa mujibu wa
mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2012, kabla ya Waziri mwenye dhamana ya
madini kubariki mauzo ya kampuni, anapaswa kupata Kibali Cha kwamba kodi
zote stahili zimelipwa.
Kibali Kwa kampuni ya mantra kilitolewa bila
kujali hitaji la kisheria na sasa kampuni hii imepewa leseni.
Maamuzi
haya ya Waziri wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi
ya Tshs 300 bilioni ambazo zingeweza kumaliza tatizo la nyumba za walimu nchi
nzima na kulipia madai yote ya walimu.
Fedha hizi zingeweza kujenga
barabara ya lami kutoka Manyoni mpaka Itigi.
Fedha zingeweza kukarabati
reli ya Kati na kuirejesha katika ubora wa unaotakiwa.
Kwa mujibu wa
kanuni za Bunge nimetaka Waziri atoe maelezo bungeni na wabunge
wajadili. Ni dhahiri kwamba serikali inayoongozwa na CCM imeamua
kumaliza utajiri wote wa nchi na kuugawa kwa wageni Kwa bei ya che.
Wananchi Ni lazima kusimama imara kukataa uporaji huu na maamuzi haya ya
kiburi Cha kudharau Bunge yaliyoyafanywa na Serikali.
0 comments:
Post a Comment