Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
WATEKAJI na watesaji wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini,
Dk. Stephen Ulimboka, na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom
Kibanda, wanaendelea kuwa kitendawili baada ya Jeshi la Polisi kudai
linaendelea na uchunguzi.
Wakata jeshi hilo likishindwa kuwatia mbaroni watesaji wa wanataaluma
hao, limetamba kukamilisha uchunguzi wake kuhusu kesi inayomkabili
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai, Isaya Mungulu, kwa waandishi wa habari jana, jalada hilo
limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Licha ya matukio ya Ulimboka na Kibanda kutokea muda mrefu
ikilinganishwa na lile la Lwakatare, Mungulu alishindwa kujibu maswali
ya waandishi kuhusu suala ambalo linaonekana kupigwa danadana.
Dk. Ulimboka alitekwa na kuteswa vibaya kwa kuumizwa sehemu mbalimbali
za mwili na kung’olewa meno, kucha kisha kutelekezwa katika Msitu wa
Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Juni
26, 2012.
Katika tukio linalofanana na hilo, Kibanda naye alivamiwa wakati
akiingia nyumbani kwake na kupigwa kwa nondo kichwani, kutobolewa jicho
la kushoto, kung’olewa kucha, meno mawili na kukatwa kidole.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na
makao makuu limeunda timu za wataalamu kuchunguza matukio hayo lakini
hadi leo zimekuwa zikipigwa danadana ya kuwakamata wahusika.
Katika mkutano wake na wanahabari, Mungulu aligusia matukio hayo kwa kifupi akisema uchunguzi bado unaendelea.
“Kuhusu kuvamiwa, kuteswa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji
wa New Habari 2006, Kibanda, tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk.
Ulimboka, matukio yaliyotokea Zanzibar, uchunguzi bado unaendelea na uko
katika hatua mbalimbali ambazo kwa sasa hakuna umuhimu wa kuziweka wazi
kuepusha kuharibu upelelezi,” alisema.
Alipoulizwa ni kwa nini hawajamkamata mtuhumiwa mwingine zaidi ya yule
aliyejisalimisha katika kitubio kanisani, Joshua Mulundi, Mungulu
alikwepa akiwataka waandishi wasome nakala ya tamko la jeshi hilo.
Hata hivyo nakala hiyo iliyogawiwa haikusema chochote kuhusu tume hiyo kupata watuhumiwa wengine kwa kesi ya Dk.Ulimboka.
Tukio la Ulimboka ni kama jeshi la polisi limeinua mikono kwani
Inspekta Mkuu wa Polisi (IGP), Said Mwema, aliwahi kusema mbele ya wakuu
wenzake wa mataifa mbalimbali kuwa ni siri ya taifa.
Dk. Ulimboka mwenyewe baada ya matibabu yake nje ya nchi, hajawahi
kuhojiwa na jeshi la polisi licha ya kukaririwa na vyombo vya habari
akimtaja mtumishi moja aliyedai ni wa Ikulu akidai alihusika kumteka na
kumtesa.
Wakati huo huo, Mungulu alisema kuwa upelelezi wa kumwagiwa tindikali
kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha, katika uchaguzi mdogo wa
ubunge Jimbo la Igunga mkoani Tabora September 2011, upo katika hatua
za mwisho.
Alisema ingawa watuhumiwa wawili tayari wamefikishwa
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment