Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Dk. Shein aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya Chama katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Chama Mjini.
Makamo
Mwenyekiti huyo alieleza kuwa amani na utulivu ndio msingi wa mafanikio
na ndio maana chama hicho cha CCM kimekuwa kikisimamia na kudumisha
jambo hilo kwa kutambua umuhimu wake.
Alisisitiza
kuwa tayari Zanzibar imeshajijengea sifa kubwa Kimataifa kutokana na
mafanikio makubwa yaliopatikana katika kuimarisha na kuiendeleza
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, hivyo
kujitokeza kwa watu wachache kutaka kuvuruga amani serikali
haitowafumbia macho.
Alieleza
kuwa wananchi wote wa Zanzibar wana haki sawa na ndio maana Serikali
anayoiongoza chini ya chama cha Mapinduzi haimbagui mtu kwa jinsia,
rangi, dini ama ukabila.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyo na mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa haitomvumilia mtu yeyote atakaevuruga amani na utulivu uliopo nchini.
Katika
hotuba zake, Dk. Shein aliwasisitiza wanaCCM kuendeleza utamaduni wao
wa kuimarisha amani na utulivu na kuzidisha mashirikiano kwani ndio ngao
ya ushindi wa chama hicho.
Aidha,
Dk. Shein alisisitiza kuwa Serikali anayoiongoza itaendelea kuyalinda
na kuyadumisha Mapinduzi ya Januari 12, 1964 sanjari na kuulinda
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mapema
Dk. Shein alipokea taarifa ya kazi za Chama ya Mkoa wa Mjini na baada
ya hapo alifika Kisiwandui na kwa ajili ya kuzindua rasmi Benki ya
SACCOS ya Umoja wa Wajasiriamali wadogowadogo na kueleza kuwa hatua hiyo
ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Baada
ya hapo Makamu huyo wa CCM Zanzibar alikwenda Vikokotoni kwa ajili ya
kuweka jiwe la msingi jengo jipya la ghorofa mbili la Tawi la CCM
Vikokotoni lililojengwa kwa ubia kati ya Tawi na mfanyabiashara.
Dk.
Shein alimalizia ziara yake kwa Wilaya ya Mjini, Dk. Shein alitembelea
maskani ya Kisonge iliyopo Michenzani na kuangalia uharibifu uliotokea
baada ya kuchomwa moto kwa maskani hiyo wakati wa vurugu zilizotokezea
hivi karibuni na kusababisha hasara kubwa ya zaidi ya milioni 50.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwakabidhi kadi wanachama wapya 270
kutoka Jumuiya zote za CCM zikiwemo wazazi, Umoja wa Wanawake na UVCCM
na baadae alisalimiana na wana CCM na kuwataka wanaCCM kuwafundisha
siasa vyama vyengine ambavyo vimeonesha kutoelewa maana na umuhimu wa
amani na utulivu.
Katika
ziara hiyo burudani mbali mbali zilitumbuiza zikiwemo ngoma, nyimbo,
mashairi, tenzi pamoja na burudani maalum iliyotolewa na vijana
wa CCM kutoka Ilala, Dar-es-Salaam waliyoitoa katika viwanja vya
Kisonge mjini Zanzibar. Ziara hiyo itaendelea kesho katika Wilaya ya
Amani.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment