Jaji Robert Makaramba
Imeelezwa kuwa Tanzania imekuwa ikiingia mikataba mibovu ambayo imekuwa ikiliingizia taifa hasara kutokana na wanasheria wake kutokuwa na elimu ya masuala ya mikataba pamoja na suala la mashauri ya usuluhishi ya kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa na jaji mfawidhi wa divisheni ya biashara ya mahakama kuu ya Tanzania Robert Makaramba wakati akifungua mafunzo ya mashauri ya usuluhishi ya kimataifa kwa mawakili wa serikali jijini Dar es Salaam.
Jaji Makaramba amesema kuwa Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuona rasilimali muhimu zikishindwa kuleta maendeleo ya uchumi nchini na badala yake kutumiwa na wageni kwa maendeleo ya nchi zao.
Chimbuko la suala hili linaelezwa kuwa ni kutokuwa na elimu ya kutosha kwa wanasheria na mawakili wa serikali katika masuala ya mikataba na mashauri ya usuluhishi ya kimataifa.
Kutokana na hilo ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mafunzo ya masuala hayo katika shule ya sheria nchini kwa lengo la kuimarisha taaluma hiyo na kulisaidia taifa.
Wanahabari kote nchini wanainza wiki ya kutafakari na kutathmini Dhana ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo huadhimishwa kila ifikapo terehe 3 ya mwezi wa tano kila mwaka.
Siku ya uhuru wa vyombo vya habari ilianza kusikika tangua karne ya 15 mpaka 16 kwa lengo la kuleta ukombozi wa uhuru dhidi ya uandishi wa habari .
Kwa mujibu wa mkufunzi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ayoub Ryoba anaeleza kuwa uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini Tanzania ulianza kuchukua kasi mwanzoni mwa miaka ya themanini .
Hata hivyo wakati harakati hizo zikiendelea takwimu zinaonyesha kuwa bado wanahabari wengi bado wanazibwa midomo au kupoteza maisha kutoka na kile wanachokiandika au kukiamini.
Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwak ahuu yatafanyika jijini Arusha ambapo pia kutazinduliwa mfuko wa kumkumbuka mwandishi David mwangosi aliyefariki dunia mwaka jana wakati akiwa kazini.
0 comments:
Post a Comment