Latest News

Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya  katiba,  Jaji Joseph Sinde Warioba

Tume ya mabadiliko ya katiba  nchini imewataka watanzania kukubali na kupokea maamuzi magumu yatakayotolewa  na tume hiyo wakati wa  kutoa rasimu ya uundwaji wa katiba mpya  kwa wananchi ambayo  inatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.

Akitoa taarifa ya tathimini  ya kazi mbalimbali ya tume ya mabadiliko ya  katiba  ya uundwaaji wa mabaraza ya katiba ya wilaya na serikali za mitaa,  mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa tume iko tayari kufanya maamuzi magumu na kuwaomba wananchi nao kuwa tayari.
 
Jaji Warioba amesema katika zoezi hilo, tume imekabiliana na changamoto kadhaa zikiwemo za vitendo vya rushwa, udini na siasa lakini akasisitiza kuwa  kuwa katiba itakayotengenezwa itakuwa ya
watanzania wote na si ya  kikundi flani.

Tathimini ya  tume hiyo inaonyesha kuwa  asilimia 99.8 ya kata zote za Tanzania bara zimepitiwa katika uundwaji wa  mabaraza ya katiba huku asilimia 96.4 ya shehia visiwani Zanzibar zikifanikiwa kuunda mabaraza.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top