Waziri wa Ujenzi, Dkt. Jphn Magufuli
 Wizara ya ujenzi na wakala wa majengo Tanzania (TBA),   imewafukuza kazi na kusitisha mikataba ya wafanyakazi waandamizi saba kwa tuhuma za ubadhirifu na utendaji kazi mbaya.
 
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msemaji wa wizara M.S Martin , imeeleza kuwa waziri wa ujenzi Dr. John Magufuli amekuwa akipokea taarifa za vitendo vya ubadhirifu miongoni mwa watendaji waandamizi katika wakala zinazotoa huduma chini ya wizara hiyo.
 

Waliofukuzwa kazi ni pamoja na aliyekuwa meneja wa TBA mkoa wa Dar es Salaam, wahasibu wasaidizi mkoa wa Dar es Salaam, mkurugenzi wa biashara na fedha pamoja na mhandisi wote kutoka mkoani Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imesema hatua hizo zilizochukuliwa ni mwendelezo wa juhudi za wizara hiyo kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayoashiria kuwepo utendaji unaokiuka maadili .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top