Serikali imejipanga kutoa elimu jumuishi kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kutoa fursa sawa kwa kujenga miundo mbinu rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa elimu maalum kutoka wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii Benjamini Kurwa amesema kuwa katika mpango wa elimu jumuishi watoto wenye ulemavu watapewa fursa ya kushiriki katika shule za kawaida.
Mkurugenzi huyo amesema majengo yanakarabatiwa ili kuweka mazingira rafiki kwa kila mwanafunzi kujifunza katika shule huku akisema shule mpya zitajengwa kwa mifumo bora yenye miundo stahiki.
Wizara inaandaa walimu wa kutosha ambao ni wa elimu maalum na walimu wa shule za kawaida ili kuhudumia halmashauri 77 na wanafunzi elfu 24 wenye mahitaji maalum.
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na vyama vya watu wenye ulemavu ili waweze kujua idadi kamili ya mahitaji ya wanafunzi kwa ajili ya kuwaingiza katika mpango wa elimu jumuishi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment