MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI
KAMISHINA WA POLISI ZANZIBAR
MAKAO MAKUU YA POLISI ZANZIBAR
29.03.2013
Ndugu waandishi wa habari,
Assallam Aleykum
Ahsanteni.
Ijumaa karimu.
MUSSA A. MUSSA - CP
KAMISHNA WA POLISI
ZANZIBAR
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Assallam Aleykum
Najua
leo ni siku ya mapumziko na siku ya ibada kwa waumini wote. Leo tupo
katika Ijumaa Kuu lakini pia ni siku ya sala ya pamoja kwa Waislam
katika misikiti mbalimbali. Nimeamua tukutane leo kwa sababu tatu.
Kwanza kwa kuendelea kudumisha doria za mjini na vijijini kwa kutumia
gari, Askari wa miguu, pikipiki na mbwa ili kuhakikisha usalama unadumu
Visiwani hapa.
Tunaendelea kutoa ushauri wa kiusalama na kushirikiana
kwa karibu zaidi na wananchi wote kuona maisha na mali zao zinakuwa
salama. Tunawaomba wenye mahoteli ya kitalii na nyumba za starehe kuwa
karibuna jeshi lao la Polisi pamoja na kufuata ushauri wote wa
kiusalama wanaopewa kila wakati.
Pili tumeitana hapa kutoa shukurani kwa wananchi wote. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote kwa ujumla wao kwa ushirikiano mkubwa mnaotupa. Si rahisi kutaja kila msaada tunaopata kutoka makundi mbalimbali ya wananchi wteu, lakini tukiri msaada tunaopata ni mkubwa na umetusaidia na unaendelea kutusaidia katika kudumisha amani na utulivu.

Hata hivyo, napenda kutoa
shukurani zangu za dhanti kwa nyinyi waandhishi wa habari hasa wa ahapa
Zanzibar kwa kuwa karibu na ofisi yangu na kuchangia kwa kiwango kikubwa
mchakato mzima wa kudumisha amani Visiwani hapa.
Jambo la tatu tuliloitania hapa ni kupeana taarifa juu ya maendelea ya kesi ya mauaji ya Padri Evarest Mushi. Najua si nyinyi tu waandishi wa habari lakini Watanzania wote wanataka kujua maendeleo ya upelelezi wa tukio hili. Jeshi la Polisi liliwaahidi litawajulisha kila hatua iliyofikiwa juu ya upelelezi wa shauri hili.

Mpaka hapa tunapozungumza upelelezi wa shauri
hili umefikia pahala pazuri na jalada la shauri hili limeshapalekwa kwa
Mkurugenzi wa Mashitaka kwa hatua za kisheria. Muhusika wa mauaji haya
tayari amekamatwa na ametambuliwa na watu walioshuhudia tukio hilo.
Mtakumbuka Jeshi la Polisi mbali na hatua kadhaa za kiupelelezi
walizozichukua ilikuwa ni pamoja na kuchora michoro ya sura ya mtu kwa
kutumia watu walioshuhudia tukio hilo. Baada ya kuitoa picha hiyo
katika vyombo vya habari mabalimbali vya kiulinzi, wananchi, vyombo vya
habari na mitandao ya kijamii muhalifu huyo ametambulika na kutambuliwa.
Jeshi la Polisi liliahidi kutoa milioni kumi kwa watu watakaosaidia kupatikana kwa muhalifu huyo. Ahadi ile ipo pale pale na mwananchi aliyesaidia kutoa utambuzi Jeshi la Polisi litamzawadia kiwango hicho cha fedha, laini kwa usalama wa shahidi huyo na kwa sababu za kiupelelezi tukio la kumkabidhi fedha hizo hatutaliweka bayana katika vyombo vya habari.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha upelelezi wa matukio mengine yaliyopita. Tunawaahidi kuendelea kuwasisitiza na kutotoa siri wala kuwataja wale wote wanaotupa taarifa za kihalifu.
Mwisho kabisa, naomba niwashukuru tena wananchi wote wa Zanzibara kwa kuwa karibu na ofisi yangu na Jeshi la Polisi kwa ujumla katika mapambano ya vitendo vya kihalifu.

1 comments:
Kazi nzuri ila itufikishe mpaka mwisho wa mchezo na matokeo tuyaone isiwe kiini macho
Post a Comment